Nafasi ya Kazi: Dereva Ubalozi wa Uingereza Dodoma
Ubalozi wa Uingereza (British High Commission) mjini Dodoma unatangaza nafasi ya ajira kwa cheo cha Dereva S1 kwa mkataba wa miezi 12. Mtu atakayepata nafasi hii atawajibika kusafirisha wafanyakazi wa ubalozi na wageni waliothibitishwa ndani ya Tanzania kwa kufuata viwango vya usalama na sera za usafiri za FCDO na BHC.
Eneo la kazi: Dodoma, Tanzania
Mshahara: TZS 1,122,417 kwa mwezi
Muda wa kazi: Saa 35.5 kwa wiki
Tarehe ya kuanza kazi: 1 Oktoba 2025
Mwisho wa kutuma maombi: 19 Agosti 2025
Miongoni mwa majukumu ni pamoja na kuendesha magari ya ubalozi, kusaidia shughuli za ofisi, kushughulikia barua pepe, na kutoa msaada wa huduma ya kwanza. Waombaji wanapaswa kuwa na cheti cha udereva, uzoefu wa angalau miaka 3, na uwezo wa kuzungumza Kiingereza na Kiswahili kwa ufasaha.
Jinsi ya kutuma maombi:
Tembelea kiungo hiki:
🔔 Je, unatafuta Nafasi za Kazi? Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya ajira kila siku!
🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya za ajira kila siku!