NAFASI Za Kazi BRAC Tanzania Finance Limited
BRAC Tanzania Finance Limited (BTFL) ni sehemu ya mtandao mkubwa wa maendeleo duniani, ukiwa na miradi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi katika bara la Asia na Afrika. Hapa nchini, BTFL imejikita katika kutoa mikopo midogo hadi ya kati, ikihudumia Watanzania kupitia matawi zaidi ya 150 yaliyopo katika mikoa 25.
BTFL ni moja ya taasisi zinazoongoza katika huduma za kifedha kwa wananchi wa kipato cha chini, hasa maeneo ya vijijini. Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 55 ya wateja wake wanatoka vijijini, huku zaidi ya asilimia 98 wakiwa ni wanawake – jambo linaloonesha kujitolea kwao katika kuinua uchumi wa wanawake wa Tanzania.
Kwa sasa, BTFL imetangaza nafasi mpya za ajira kwa watanzania wenye sifa stahiki. Shirika hili linaamini katika usawa wa kijinsia na fursa kwa wote bila kujali asili, jinsia au hali yoyote ya kijamii. Waombaji wote wanaohitaji nafasi hizi wanahimizwa kutuma maombi kwa uharaka na kwa kufuata maelekezo yaliyo kwenye tangazo rasmi.
Jinsi ya Kupata Taarifa Kamili
Orodha ya nafasi zote zinazopatikana kwa sasa imeambatanishwa kwenye waraka wa PDF.
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA TANGAZO
🔔 Unatafuta Nafasi za Kazi? Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya ajira kila siku!
🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!