Nafasi za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe Zatangazwa Rasmi
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe inakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na vigezo vya kitaaluma kwa ajili ya kujaza nafasi za ajira za mkataba katika idara za Radiografia na Mapokezi. Waombaji wenye nia ya kuhudumu katika taasisi hii ya afya ya mkoa wanapaswa kuwasilisha maombi yao kabla ya tarehe 15 Agosti 2025.
Nafasi Zinazopatikana
Mteknolojia wa Mionzi Daraja la II β Nafasi 2
Sifa za Kuajiriwa
Muombaji anapaswa kuwa na stashahada katika fani ya Radiografia kutoka chuo kinachotambulika na Serikali, na awe amesajiliwa na Baraza la Radiolojia na Picha za Kimatibabu (Medical Radiology and Imaging Professional Council).
Majukumu ya Kazi
- Kutunza mitambo ya Radiotherapia na kuhakikisha ufanisi wake
- Kufanya vipimo vya mionzi kwa wagonjwa
- Kusimamia ubora wa mionzi kutoka kwa mitambo ya tiba
- Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu huduma za mionzi
- Kusimamia vifaa vya tiba na usafi wa mazingira ya kazi
- Kutoa mafunzo kwa watumishi wapya
- Kufanya majukumu mengine atakayopangiwa
Afisa Mapokezi Daraja la II β Nafasi 3
Sifa za Kuajiriwa
Muombaji anapaswa kuwa na stashahada katika fani ya mapokezi au huduma kwa wateja kutoka chuo kinachotambulika na Serikali, pamoja na ujuzi wa matumizi ya kompyuta.
Majukumu ya Kazi
- Kutunza kumbukumbu na taarifa za wagonjwa
- Kupokea na kuelekeza wagonjwa pamoja na wageni
- Kufungua faili za wagonjwa na kudhibiti taarifa zao kwa usiri
- Kuwasiliana na wodini na kuhakikisha taarifa za wagonjwa zinasasishwa
- Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa kulingana na uzoefu na taaluma yake
Masharti ya Jumla kwa Waombaji
- Awe na umri usiozidi miaka 35 na mwenye afya bora
- Awasilishe CV, barua mbili za wadhamini (watumishi wa umma) zenye mawasiliano ya uhakika
- Aambatishe vyeti halisi vilivyothibitishwa (si “statement of results” au “provisional”)
- Kwa waliohitimu nje ya nchi, vyeti viwe vimehakikiwa na NECTA au TCU
- Vyeti vya lazima ni:
- Cheti cha kuzaliwa
- Cheti cha kidato cha nne na sita (kwa waliomaliza)
- Cheti cha taaluma na leseni ya kitaaluma
- Cheti cha kompyuta
- Picha moja ya pasipoti
Jinsi ya Kutuma Maombi
Waombaji wanapaswa kutuma maombi kwa njia ya posta au kufikisha moja kwa moja katika anuani ifuatayo:
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe
S.L.P 1044
Njombe
Mwisho wa kutuma maombi: 15 Agosti 2025
π Tafuta Nafasi za Kazi? Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya ajira kila siku!
π Tembelea Habari Wise kwa habari mpya za ajira kila siku!