Nafasi za Kazi Kairuki Hospital Tanzania 2025
Hospitali ya Kairuki iliyopo Mikocheni, Dar es Salaam, inakaribisha maombi kutoka kwa waombaji wenye sifa, uzoefu na uwezo wa kitaaluma kujaza nafasi zifuatazo:
1. Marketing & Public Relations Manager (Nafasi 1)
Mahali: Mikocheni, Dar es Salaam
Aina ya Ajira: Muda Wote
Idara: Marketing and PR
Anaripoti Kwa: Director General
Majukumu:
- Kuandaa na kusimamia mikakati ya masoko na PR ili kuimarisha jina, taswira na ushirikiano wa hospitali na jamii.
Sifa:
- Shahada ya Masoko, PR, Mawasiliano au taaluma inayohusiana (Shahada ya Uzamili inapendelewa).
- Uzoefu wa angalau miaka 5 kwenye PR/Masoko, hususan sekta ya afya.
- Uwezo mzuri wa mawasiliano, uhusiano na vyombo vya habari pamoja na ujuzi wa digital marketing.
2. Digital Communication Officer (Nafasi 1)
Mahali: Mikocheni, Dar es Salaam
Aina ya Ajira: Muda Wote
Anaripoti Kwa: Marketing and PR Manager
Majukumu:
- Kusimamia mikakati ya mawasiliano ya kidijitali ya hospitali ili kuongeza mwonekano wa chapa na ushirikiano na jamii.
Sifa:
- Shahada ya Mawasiliano, Digital Marketing, Uandishi wa Habari au taaluma inayohusiana.
- Uzoefu wa angalau miaka 3 kwenye digital communications/social media.
- Ujuzi wa graphic design, multimedia editing, CMS, analytics tools, na SEO/SEM.
3. Dereva (Nafasi 1)
Mahali: Mikocheni, Dar es Salaam
Aina ya Ajira: Muda Wote
Anaripoti Kwa: Transport Officer / Head Driver
Majukumu:
- Kusafirisha wagonjwa, vifaa na dawa kwa usalama na kwa wakati.
Sifa:
- Elimu ya Sekondari (Kidato cha Nne) + Cheti cha Udereva kutoka NIT.
- Uzoefu wa angalau miaka 2 katika udereva, inapendelewa kwenye sekta ya afya.
- Leseni halali ya udereva, rekodi safi; cheti cha huduma ya kwanza kitapewa kipaumbele.
Jinsi ya Kutuma Maombi
- Andika barua ya maombi ikielekezwa kwa Director General, Kairuki Hospital, Dar es Salaam.
- Ambatanisha CV iliyosasishwa, vyeti vya taaluma/professional vilivyothibitishwa, ushuhuda na mawasiliano ya waamuzi wawili (referees).
- Tuma maombi kupitia barua pepe: [email protected]
- Weka jina la nafasi unayoomba kwenye subject line ya barua pepe.
- Ni waombaji waliochaguliwa pekee watakaowasiliana.
📌 Mwisho wa kutuma maombi: 13 Septemba 2025, saa 10:30 jioni.