Nafasi za Kazi za Muda kwa Uchaguzi Mkuu 2025 Zanzibar Zatangazwa
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar imetangaza fursa za ajira za muda kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. Nafasi hizo ni kwa Watanzania wanaotaka kushiriki kama wasimamizi, wasimamizi wasaidizi, au makarami waongozaji katika vituo vya kupigia kura. Ajira hizi ni kwa ajili ya kusaidia zoezi la upigaji kura katika visiwa vya Unguja na Pemba.
Nafasi Zilizotangazwa
Tume imetangaza nafasi zifuatazo kwa waombaji wenye sifa stahiki:
- Wasimamizi wa Vituo vya Kupigia Kura
- Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo vya Kupigia Kura
- Makarani Waongozaji Wapiga Kura
Sifa za Waombaji kwa Wasimamizi na Wasaidizi wa Uchaguzi Mkuu Zanzibar
Waombaji wa nafasi za usimamizi wanapaswa kuwa na vigezo vifuatavyo:
- Awe raia wa Tanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18.
- Asiwe kiongozi wa chama cha siasa.
- Awe na maadili, utii, na akili timamu.
- Awe na elimu ya kidato cha nne au zaidi, na aweze kusoma na kuandika kwa Kiswahili au Kiingereza.
- Aweze kusoma na kuelewa maelekezo ya usimamizi wa vituo vya kupigia kura.
- Awe mkazi wa Shehia au Wilaya anayoomba kufanya kazi.
Sifa za Waombaji wa Karani Waongoza Wapiga Kura
Kwa nafasi ya karani mwongozaji, waombaji wanapaswa kuwa:
- Raia wa Tanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18.
- Asiwe kiongozi wa chama cha siasa.
- Mwenye tabia njema na uwezo wa kufuata maagizo.
- Aliyemaliza kidato cha nne au zaidi na anayejua kusoma na kuandika kwa Kiswahili au Kiingereza.
- Mwenye uwezo wa kuelewa maelekezo ya kazi ya karani.
- Mkazi wa eneo analoomba kufanyia kazi.
Masharti ya Jumla kwa Waombaji
- Mwombaji ni lazima aeleze wazi nafasi anayoiomba pamoja na Shehia au Wilaya anayotaka kufanyia kazi.
- Awe tayari kupangiwa kituo chochote ndani ya Wilaya anayoomba.
- Aambatishe nakala za vyeti vya elimu ya sekondari na taaluma (ikiwa anavyo).
- Awasilishe wasifu wake (CV) pamoja na anuani ya makazi, namba za simu na majina ya wadhamini wawili wenye namba za NIDA au kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi.
- Aweke picha mbili za ukubwa wa “passport size”.
- Aambatishe barua ya utambulisho kutoka kwa Sheha wa eneo analoishi.
- Watumishi wa umma wanatakiwa kupitisha barua ya maombi kwa waajiri wao.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Barua zote za maombi ziandikwe kwa anuani ifuatayo:
Mkurugenzi wa Uchaguzi
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi
Ofisi ya Zanzibar
Mtaa wa Maisara
S.L.P 4670, ZANZIBAR
Waombaji wanatakiwa kuwasilisha maombi yao katika ofisi za wasimamizi wa uchaguzi wa Wilaya husika kwa Unguja na Pemba. Maombi yasiyozingatia utaratibu hayatafanyiwa kazi.
Barua za maombi ziandikwe kwa kuonyesha nafasi inayotakiwa pamoja na Wilaya au Jimbo linaloombewa, na lazima ziambatishwe na vyeti vya elimu pamoja na CV.
Tahadhari: Mtu yeyote atakayebainika kuwasilisha taarifa za kughushi atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Mwisho wa Kutuma Maombi
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 16 Agosti 2025 saa 9:30 alasiri.
🔔 Tafuta Nafasi za Kazi? Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya ajira kila siku!
🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya za ajira kila siku!