Elimu

Nafasi za Mafunzo ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi 2025/2026 Awamu ya Pili

Nafasi za Mafunzo ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi 2025/2026 Awamu ya Pili

Nafasi za Mafunzo ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi 2025/2026 Awamu ya Pili

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) ametangaza rasmi nafasi za kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya Stashahada ya Ualimu katika Elimu ya Awali na Msingi kwa mwaka wa masomo 2025/2026, awamu ya pili. Mafunzo haya ni pamoja na Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali, Msingi na Elimu Maalumu yenye muda wa miaka 2, pamoja na Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi kwa miaka 3 katika masomo ya Sayansi na Hisabati.

Sifa za Waombaji

Waombaji wa kozi za miaka 2 ni wahitimu wa Kidato cha Sita wenye daraja la kwanza hadi la tatu (I-III). Kwa upande wa Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi (miaka 3), waombaji wanatakiwa kuwa wahitimu wa Kidato cha Nne wenye daraja la kwanza hadi la tatu (I-III) na kufaulu angalau alama ā€œCā€ katika masomo matatu, mawili kati yao yakiwa Basic Mathematics, Biology, Chemistry, Physics, Information and Computer Studies au Computer Science.

Mahali pa Mafunzo

Mafunzo yatafanyika katika vyuo vya ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali kote nchini. Wizara inahimiza waombaji wenye sifa kuzitumia nafasi hizi kujiunga na mafunzo haya.

Maelezo Zaidi Kuhusu Sifa za Kujiunga

Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi (Miaka 2)

  • Wahitimu wa Kidato cha Sita waliopata daraja la I-III na “Principal Pass” mbili.
  • Waombaji waliomasoma masomo ya Economics, Commerce, na Book Keeping wanashauriwa kuomba kozi ya Elimu ya Awali.
  • Walimu waliokamilisha kozi ya Astashahada (Cheti) ya Ualimu Elimu ya Awali au Msingi pia wanaweza kuomba.
  • Waombaji watapangwa kulingana na matokeo yao katika Mtihani wa Taifa wa Ualimu ngazi ya Astashahada.

Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi (Miaka 3)

  • Wahitimu wa Kidato cha Nne waliopata daraja la I-III na kufaulu angalau alama ā€œCā€ katika masomo muhimu.

Aina za Mafunzo na Vyuo Vinavyotoa

A. Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi (Miaka 2)

Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi (Miaka 2)
Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi (Miaka 2)
Screenshot 20

B. Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi katika Sayansi na Hisabati (Miaka 3)

Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi katika Sayansi na Hisabati (Miaka 3)
Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi katika Sayansi na Hisabati (Miaka 3)

Utaratibu wa Maombi

  • Wahitimu wa Kidato cha Nne, Kidato cha Sita na walimu waliokamilisha Astashahada wanaweza kutuma maombi ikiwa wanakidhi sifa.
  • Maombi ya vyuo vya Serikali yatapokelewa kupitia mfumo wa mtandao wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia https://tcm.moe.go.tz/.
  • Waombaji wa kozi ya miaka 2 watatakiwa kuchagua kozi tatu kwa kuanzia na ile wanayopendelea zaidi.
  • Waombaji wa kozi ya miaka 3 watachagua tahasusi tatu kwa mpangilio wa upendeleo.
  • Majibu ya maombi ya vyuo vya Serikali yatatolewa kupitia akaunti za mtandao kuanzia tarehe 18/08/2025 na pia kupitia vyuo vilivyoteuliwa.
  • Maombi kwa vyuo visivyo vya Serikali yatawasilishwa moja kwa moja kwa vyuo husika na majibu yatatolewa na vyuo hivyo.
  • Fomu za maombi zinapatikana kupitia tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia www.moe.go.tz pamoja na chuo kitakachomchagua mwombaji.
  • Waombaji wanashauriwa kutoa taarifa kamili za mawasiliano ikiwemo barua pepe na namba ya simu kwa urahisi wa mawasiliano.
  • Mwisho wa kuwasilisha maombi ni tarehe 14/08/2025.

šŸ”” Kwa habari mpya Kila siku. Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya habari kila siku!
🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!