Nafasi za Ufadhili wa Masomo Mwalimu Nyerere Memorial Academy University 2025/2026
Mfuko wa Udhamini wa Kumbukumbu ya Mwalimu Julius K. Nyerere umetangaza rasmi nafasi kumi (10) za ufadhili wa masomo kwa mwaka wa 2025/2026. Mfuko huu ulianzishwa tarehe 12 Oktoba 2009 na Benki Kuu ya Tanzania kuenzi mafanikio ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere.
Lengo la Mfuko wa Udhamini
Mfuko huu umejitolea hasa kufadhili wanafunzi wa kike wenye matokeo bora wanaosoma shahada ya kwanza katika fani za Sayansi na Hisabati katika vyuo vikuu vinavyotambulika nchini Tanzania, ili kukuza ubora wa kitaaluma katika nyanja hizi.
Fani Zinazofadhiliwa
Mbali na wanafunzi wa kike, ufadhili pia unapatikana kwa wanaume na wanawake wanaosoma shahada ya kwanza katika fani za Sayansi, Hisabati, Uchumi, Teknolojia ya Habari, Uhasibu na Fedha.
Vigezo vya Ufadhili
Scholarships hutolewa kwa kuzingatia sifa bora za kitaaluma na kupitia mchakato mkali wa uteuzi. Waombaji waliopitishwa hupata udhamini kamili unaojumuisha ada za masomo pamoja na gharama nyingine muhimu kama chakula, malazi, posho ya vitabu, vifaa vya kuandikia, mafunzo ya vitendo, mahitaji maalum ya kitivo, na hata kompyuta mpya kabisa kama inavyoainishwa na taasisi husika.
Maelezo Zaidi na Maombi
Udhamini huu umefafanuliwa zaidi katika PDF rasmi inayopatikana kupitia link ifuatayo. Waombaji wanahimizwa kupakua tangazo na fomu za kujiunga.
BOFYA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA TANGAZO NA FOMU ZA KUJIUNGA
🔔 Kwa habari mpya Kila siku. Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya habari kila siku!
🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!