Michezo

Neo Maema Asaini Simba SC

Neo Maema Asaini Simba SC

Neo Maema Asaini Simba SC

Klabu ya Simba SC imetangaza rasmi kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Neo Maema akitokea Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini. Mchezaji huyo amesaini mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwaka mwingine kutegemea makubaliano.

Mchezaji Mzoefu

Neo Maema, raia wa Afrika Kusini mwenye umri wa miaka 29, ni miongoni mwa wachezaji wenye uzoefu mkubwa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Uwepo wake ndani ya kikosi cha Simba SC unatarajiwa kuongeza ubunifu na nguvu katika safu ya kiungo cha ushambuliaji.

Usajili wa Maema unaongeza matumaini mapya kwa mashabiki wa Simba SC, klabu inayolenga kufanya vizuri kwenye ligi ya ndani na mashindano ya kimataifa msimu wa 2025/2026.