Michezo

Neymar Aachiwa Urithi wa Trilioni 2.5 na Bilionea Asiyemjua

Neymar Aachiwa Urithi wa Trilioni 2.5 na Bilionea Asiyemjua

Neymar Aachiwa Urithi Mkubwa Brazil

Kumekuwepo na simulizi ya kushangaza nchini Brazil baada ya bilionea mwenye umri wa miaka 31 kutoka jimbo la Rio Grande do Sul kuamua kumwachia nyota wa soka Neymar Jr mali zake zote, ingawa wawili hao hawakuwa na uhusiano wowote wa karibu wala kukutana ana kwa ana.

Thamani ya Urithi

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya kimataifa, kijana huyo tajiri hakuwa na mke wala watoto. Mwezi Juni 2025 aliandika wosia rasmi serikalini mbele ya mashahidi akielekeza majumba, kampuni na vitega uchumi vyake vyote vyenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 1 (sawa na shilingi trilioni 2.5 za Kitanzania) viende kwa Neymar pekee.

Sababu za Uamuzi

Sababu kuu iliyoelezwa ni heshima kubwa aliyokuwa nayo kwa utu wa Neymar, akivutiwa na unyenyekevu wake pamoja na ukaribu wake na baba yake. Tabia hizo zilimshawishi bilionea huyo kufanya uamuzi wa kipekee wa kumwachia staa huyo mali zote.

Hatua Zinazofuata

Kwa sasa, urithi huo mkubwa unasubiri mchakato wa kisheria kupitia mahakama za Brazil kabla ya kuhamishiwa rasmi kwa Neymar, ambaye anakipiga katika Santos FC na timu ya taifa ya Brazil.

Neymar Aachiwa Urithi Mkubwa Brazil