Ousseini Badamassi: Profaili ya Kiungo wa TP Mazembe Anayetakiwa Simba
Tetesi za usajili Simba SC zimezidi kushika kasi kuelekea msimu wa 2025/2026, na jina moja limekuwa likitajwa mara kwa mara katika vichwa vya habari: Ousseini Soumaila Badamassi. Kiungo huyu mwenye umri wa miaka 28, raia wa Niger na anayekipiga katika klabu kubwa ya Afrika, TP Mazembe, anaripotiwa kuwa kwenye rada za miamba hiyo ya Msimbazi, huku mashabiki wakitamani kuona damu mpya na vipaji vya kimataifa vikijiunga na kikosi chao.
Badamasi, aliyezaliwa Niamey mnamo Aprili 21, 1997, amejijengea sifa kubwa kama kiungo wa kati (Central Midfield) kutokana na uwezo wake mkubwa wa kumiliki mpira, kupiga pasi za uhakika, na kujenga mashambulizi kutoka katikati ya uwanja. Uzoefu wake wa kucheza katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na uwezo wake wa kusaidia timu yake katika nyanja zote za kiungo unamfanya kuwa chaguo la kuvutia kwa benchi la ufundi la Simba SC, ambalo linatafuta kuimarisha safu yake ya kati ili kukabiliana na changamoto za Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano ya kimataifa.
Usajili Simba 2025/26: Ousseini Badamassi Kipaumbele cha Wekundu?
Katika usajili Simba 2025/2026, uongozi wa klabu unatarajiwa kufanya maboresho makubwa ili kuhakikisha wanarudisha hadhi yao ya kuwa tishio barani Afrika. Kuongezwa kwa kiungo kama Badamasi, ambaye amekuwa aking’ara na TP Mazembe, kunaweza kuleta mabadiliko makubwa katika mfumo wa uchezaji wa Simba, kutoa pumzi mpya kwa viungo waliopo, na kuongeza ushindani ndani ya kikosi. Wakala wake, AGBEVE KSPORTS, bila shaka atakuwa na kazi kubwa ya kufanya ikiwa tetesi hizi zitaendelea kushika kasi.

Ingawa bado hakuna tamko rasmi kutoka pande zote mbili, tetesi hizi zinaendelea kuwafanya mashabiki wa Simba SC wawe na hamu kubwa ya kujua hatma ya Badamasi. Je, kiungo huyu mahiri atatua Msimbazi na kuwa seheamu ya historia mpya ya Simba? Wakati utaamua.
Habari za usajili Simba SC 2025/2026 zinamhusisha Ousseini Badamasi. Kiungo huyu hatari wa TP Mazembe anaweza kuongeza nguvu Msimbazi.
🔔 Je? unatafuta Nafasi za Kazi? Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya ajira kila siku!
🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!