Ratiba ya CAF Champion League na CAF Confederation Cup 2025/2026
Droo ya raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika kwa msimu wa 2025/2026 inatarajiwa kufanyika leo Agosti 9, saa 8 mchana nchini Tanzania. Dhamira ni kuanzisha rasmi mashindano haya makubwa ya CAF kwa msimu huu.
Wawakilishi wa Tanzania
Tanzania itawakilishwa katika Ligi ya Mabingwa na vilabu vya Simba SC na Yanga SC, huku Azam FC na Singida Black Stars wakijiandaa kushiriki Kombe la Shirikisho. Hii ni fursa kubwa kwa timu hizi kuonyesha ubora wa soka la Tanzania barani Afrika.
Ratiba ya Mashindano
Raundi ya Kwanza ya Awali
- Mechi za nyumbani na ugenini: 19–28 Septemba 2025
Raundi ya Pili ya Awali
- Mechi za nyumbani na ugenini: 17–26 Oktoba 2025
Hatua ya Makundi
- Kuanzia Novemba 2025 hadi Februari 2026
Robo Fainali
- Kuanzia Machi 2026
Nusu Fainali
- Kuanzia Aprili 2026
Fainali
- Kati ya Mei 8 hadi Mei 24, 2026
🔔 Kwa habari mpya za Michezo. Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya michezo kila siku!
🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!