Ratiba Rasmi ya Mechi za Playoff Ligi Kuu Tanzania 2024/2025
Ratiba ya Mechi za Playoff Ligi Kuu Tanzania: Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Bodi ya Ligi (TPLB) limetoa ratiba kamili ya mechi za mtoano zitakazoamua timu zitakazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2025/2026. Michuano hii ni ya kuamua hatma ya timu zilizoshika nafasi za chini katika msimamo wa mwisho wa NBC Premier League pamoja na washindi wa Ligi Daraja la Kwanza.
Tarehe | Mechi | Hatua ya Mchezo |
---|---|---|
Juni 25, 2025 | Tanzania Prisons vs Fountain Gate | Ligi Kuu (Leg 1) |
Juni 29, 2025 | Fountain Gate vs Tanzania Prisons | Ligi Kuu (Leg 2) |
Julai 03, 2025 | Mshindi wa Ligi Kuu vs Stand United | Playoff ya Mwisho (Leg 1) |
Julai 07, 2025 | Stand United vs Mshindi wa Ligi Kuu | Playoff ya Mwisho (Leg 2) |
Raundi ya Kwanza ya Playoff – Juni 25 na 29, 2025
Katika hatua ya kwanza ya mtoano, Tanzania Prisons na Fountain Gate zitachuana katika michezo miwili ya nyumbani na ugenini. Timu hizi ndizo zilizomaliza nafasi ya 13 na 14 kwenye msimamo wa mwisho wa Ligi Kuu msimu wa 2024/2025.
- Juni 25, 2025: Tanzania Prisons vs Fountain Gate (Leg 1)
- Juni 29, 2025: Fountain Gate vs Tanzania Prisons (Leg 2)
Mshindi wa jumla katika raundi hii ya kwanza atafuzu kucheza raundi ya pili ya fainali dhidi ya bingwa wa mtoano wa Ligi Daraja la Kwanza, Stand United.
Fainali ya Playoff – Julai 3 na 7, 2025
Raundi ya mwisho ya mtoano italeta pamoja mshindi kutoka hatua ya awali na Stand United. Timu hizi zitakutana kwenye mikondo miwili, ambapo mshindi atajihakikishia tiketi ya kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2025/2026.
- Julai 03, 2025: Mshindi wa Ligi Kuu vs Stand United (Leg 1)
- Julai 07, 2025: Stand United vs Mshindi wa Ligi Kuu (Leg 2)
Ratiba ya mechi za playoff format

Mechi hizi za mtoano zina umuhimu mkubwa kwa klabu shiriki, kwani ushindi katika raundi hizi mbili unamaanisha kuendelea kubaki au kupanda daraja kwenye Ligi Kuu. Kwa mashabiki na wadau wa soka la Tanzania, huu ni wakati wa kuangalia kwa karibu hatma ya timu hizo katika msimu ujao wa 2025/2026. Ratiba ya Mechi za Playoff Ligi Kuu Tanzania
🔔 Je? unatafuta Nafasi za Kazi? Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya ajira kila siku!
🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!