Michezo

Simba S.C. Wachezaji Wapya Msimu wa 2025/2026

Wachezaji Wapya wa Simba SC kwa Msimu wa 2025/2026

Orodha ya Wachezaji Wapya wa Simba SC 2025/2026

Wachezaji Wapya wa Simba SC Waliosajiliwa kwa Msimu wa 2025/2026, Simba SC, moja ya klabu kubwa barani Afrika, imeanza maandalizi ya msimu mpya wa 2025/2026 kwa kusajili nyota wapya wenye viwango vya kimataifa. Usajili huu unalenga kuimarisha kikosi chao kuelekea Ligi Kuu ya NBC pamoja na michuano ya kimataifa kama CAF Champions League.

Hii hapa ni orodha ya wachezaji wapya wa Simba SC kwa msimu wa 2025/2026:

  1. Rushine De Reuck
  2. Allasane Kante
  3. Morice Abraham
  4. Hussein Daudi Semfuko
  5. Jonathan Sowah
  6. Mohamed Bajaber
  7. Anthony Mligo
  8. Naby Camara
  9. Yakoub Suleiman
  10. Ahmed Pipino
  11. Seleman Mwalimu
  12. Neo Maema
  13. Wilson Nangu
  14. Vedastus Paul Masinde

Majina ya Wachezaji Waliosajiliwa

1. Rushine De Reuck

Beki wa kati raia wa Afrika Kusini, anayejulikana kwa ukabaji imara, uwezo wa kuongoza safu ya ulinzi, na uzoefu mkubwa kutoka kwenye ligi ya PSL.

Rushine de Reuck
Rushine de Reuck

2. Allasane Kante

Kiungo mkabaji mwenye nguvu kutoka Afrika Magharibi. Ana uwezo mkubwa wa kusoma mchezo na kukatiza mipango ya wapinzani.

Alassane Kanté
Alassane Kanté

3. Morice Abraham

Beki kinda wa Kitanzania mwenye kasi na uwezo wa kucheza nafasi nyingi za ulinzi. Anatazamwa kama mrithi wa muda mrefu wa mabeki wa sasa.

Morice Abraham
Morice Abraham

4. Hussein Daudi Semfuko

Kiungo chipukizi wa ndani mwenye kipaji kikubwa cha kupiga pasi na kudhibiti mchezo. Simba inampa nafasi ya kuonyesha uwezo wake kwenye jukwaa kubwa.

Hussein Semfuko
Hussein Semfuko

5. Jonathan Sowah

Mshambuliaji hatari kutoka Ghana, anayetajwa kuwa na uwezo mkubwa wa kufunga na kusaidia katika mashambulizi. Ametua Simba akiwa na matarajio makubwa.

Jonathan Sowah
Jonathan Sowah

6. Mohammed Bajaber

Nafasi: Kiungo Mshambuliaji
Uraia: Kenya
Sifa: Amejiunga akitokea Polisi Kenya FC, ana Kiwango cha hali ya juu sana

Mohammed Bajaber
Mohammed Bajaber

7. Wilson Nangu

Klabu ya Simba SC imemtambulisha rasmi beki wa kati Wilson Nangu akitokea JKT Tanzania FC, ambapo amesaini mkataba wa miaka mitatu. Nangu mwenye umri wa miaka 23 ni miongoni mwa wachezaji chipukizi wenye kipaji kikubwa. Mbali na kucheza kama beki wa kati, ana uwezo pia wa kutumika kwenye nafasi ya beki wa kushoto, jambo linaloongeza chaguo kwa benchi la ufundi la Simba.

Wilson Nangu Asaini Simba SC
Wilson Nangu Asaini Simba SC

8. Yakoub Suleiman

Klabu ya Simba SC imekamilisha usajili wa mlinda mlango wa Taifa Stars, Yakoub Suleiman, kutoka JKT Tanzania FC kwa mkataba wa miaka mitatu. Kipa huyo mwenye umri wa miaka 23 ndiye mlinda mlango wa kwanza wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, na usajili wake ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Simba SC baada ya makubaliano na JKT Tanzania kufikiwa.

Yakoub Suleiman Asaini Simba SC kwa Miaka Mitatu
Yakoub Suleiman Asaini Simba SC kwa Miaka Mitatu

9. Neo Maema

Klabu ya Simba SC imetangaza rasmi kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Neo Maema akitokea Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini. Mchezaji huyo amesaini mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwaka mwingine kutegemea makubaliano.

Neo Maema Asaini Simba SC
Neo Maema Asaini Simba SC

10. Anthony Mligo

Klabu ya Simba SC imeendelea kuimarisha kikosi chake kwa msimu wa 2025/26 kwa kutangaza rasmi usajili wa beki wa kushoto, Anthony Mligo, aliyekuwa akiichezea Namungo FC. Mchezaji huyo amejiunga na Wekundu wa Msimbazi kwa mkataba wa miaka mitatu.

CV ya Anthony Mligo, Beki Mpya wa Simba SC
CV ya Anthony Mligo, Beki Mpya wa Simba SC

11. Vedastus Paul Masinde

Simba SC imekamilisha usajili wa beki wa kati Vedastus Paul Masinde kutoka TMA Stars FC kwa mkataba wa miaka miwili. Mchezaji huyu chipukizi anachukuliwa kuwa moja ya vipaji vinavyoinukia kwenye soka la Tanzania.

Vedastus Paul Masinde Asajiliwa Simba SC
Vedastus Paul Masinde Asajiliwa Simba SC

Lengo la Usajili huu Mpya

Kuongeza Ushindani wa Kikosi

Simba SC imeamua kuongeza nguvu kwenye kila idara ya timu—ulinzi, kiungo na ushambuliaji—ili kuwa na kikosi chenye upana na ushindani wa kweli.

Maandalizi kwa CAF Champions League

Kwa kuzingatia matarajio ya kufanya vizuri barani Afrika, usajili wa wachezaji wenye uzoefu wa kimataifa kama De Reuck na Sowah ni ishara ya dhamira ya kweli ya Simba kutwaa taji la Afrika. Wachezaji Wapya wa Simba SC Waliosajiliwa kwa Msimu wa 2025/2026

🔔 Kwa habari mpya za Michezo. Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya michezo kila siku!
🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!