Michezo

Tetesi za Usajili NBC Premier League 2025/2026

Tetesi za Usajili NBC Premier League 2025/2026

Tetesi za Usajili NBC Premier League Tanzania Bara 2025/2026

Baada ya msimu wa 2024/2025 kumalizika kwa mafanikio kwa vilabu kama Yanga SC, sasa timu mbalimbali zinaendelea kuimarisha vikosi kuelekea msimu mpya wa 2025/2026. Yanga ilitwaa mataji yote ya ndani, hatua inayoongeza ushindani kwa klabu pinzani kwenye soko la usajili.

Dirisha la Usajili Lafunguliwa Rasmi na TFF

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilitangaza kuwa dirisha la usajili kwa Ligi Kuu ya NBC, Championship, First League, Ligi ya Vijana (U-20), na Wanawake limefunguliwa rasmi kuanzia Julai 1, 2025 hadi Septemba 7, 2025 saa 5:59 usiku. Usajili wote unafanyika kupitia mfumo wa FIFA Connect, na klabu zimetakiwa kuwasilisha nyaraka sahihi kwa wakati bila nyongeza ya muda.

Simba SC Yaanza Kwa Kishindo

Simba SC imeanza dirisha hili kwa usajili mkubwa wa kiungo wa ulinzi kutoka Guinea, Moussa Balla Conte (21), akitokea CS Sfaxien ya Tunisia. Conte alikuwa na mechi 34 msimu uliopita, akipokea kadi 7 za njano. Usajili huu umekuja baada ya kuachwa kwa Fabrice Ngoma na Augustine Okejepha. Pia, Simba imempeleka kwa mkopo mshambuliaji wake Omary Omary kurudi Mashujaa FC.

Azam FC Yafanya Maboresho Makubwa

Azam FC chini ya kocha mpya Florent Ibenge imefanya usajili wa nyota kadhaa akiwemo:

  • Aishi Manula kutoka Simba
  • Lameck Lawi kutoka Coastal Union
  • Muhsin Malima kutoka ZED FC, Misri
  • Manishimwe Djabel ambaye tayari amesaini
  • Himid Mao anayetegemewa kurejea
  • Basiala Agey na Ahmed Bakari Pipino wakiwa kwenye rada

Aidha, Azam iko kwenye mazungumzo na Clatous Chama, aliyemaliza mkataba na Yanga. Chama pia anawindwa na Zesco United ya Zambia. Msimu uliopita, alifunga mabao 6 na kutoa assists 3, na alikuwa sehemu ya kikosi kilichotwaa makombe 5.

Namungo FC Yavuna Vipaji kutoka Championship

Namungo FC imewasajili chipukizi wawili:

  • Cyprian Kipenye kutoka Songea United
  • Abdulaziz Shahame kutoka TMA FC

Wote walionyesha kiwango bora msimu uliopita na sasa wanapata fursa kwenye ligi kuu.

Singida Black Stars Yaanza Mchakato wa Usafishaji

Singida Black Stars imevunja mikataba ya wachezaji wawili wa kimataifa kutokana na kutopata nafasi ya kucheza:

  • Emmanuel Bola Labota (DR Congo)
  • Matthew Odongo (Uganda)

Hatua hiyo inalenga kutoa nafasi kwa wachezaji wapya katika kikosi cha msimu wa 2025/2026.

Taarifa zaidi kuhusu usajili na tetesi mpya zitaendelea kutolewa kadri dirisha linavyoendelea. Endelea kutembelea Habari Wise kwa kila update moto wa soka la Bongo.

🔔 Kwa habari mpya za Michezo. Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya michezo kila siku!
🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!