Tetesi Moto za Usajili Yanga SC Msimu wa 2025/2026
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC, wameanza maandalizi makubwa kuelekea msimu wa 2025/2026 kwa kufanya usajili wa kimkakati. Klabu imeanza mchakato wa kusuka kikosi imara baada ya baadhi ya nyota wake muhimu kuondoka, ikiwa ni juhudi za kuendelea kutamba ndani ya Ligi Kuu ya NBC, Kombe la Shirikisho la CRDB na michuano ya CAF.
TETESI za Usajili Yanga SC 2025/2026
Habari za usajili Yanga zimekuwa gumzo mitandaoni, huku uongozi wa klabu ukiwa kwenye harakati za kusajili wachezaji wa ndani na wa kimataifa wenye uwezo mkubwa wa kuhimili ushindani wa soka la Afrika.
Majina Mapya Yanayohusishwa na Yanga SC
Yanga SC inaonekana kuwa na mpango kabambe wa kuongeza nguvu kikosini kwa ajili ya msimu mpya. Miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kujiunga ni:
- Jonathan Sowah (Singida Black Stars)
- Feisal Salum “Fei Toto” (Azam FC, aliyewahi kucheza Yanga)
- Ecua Celestin (Zoman FC)
Fei Toto anaripotiwa kuwa ana mwaka mmoja wa mkataba Azam FC. Yanga imetajwa kutoa ofa ya Sh800 milioni pamoja na mshahara wa Sh40 milioni ili kumrejesha Jangwani.
Wachezaji Walioondoka Rasmi Yanga SC
- Stephane Aziz Ki amejiunga na Wydad Athletic Club (Morocco) kwa dau la takribani Sh2.9 bilioni. Alikuwa mhimili muhimu wa Yanga kwa misimu mitatu iliyopita na sasa anaelekea kushiriki Kombe la Klabu Bingwa Dunia.
Nyota Wanaoweza Kuondoka Muda Wowote
- Jonas Mkude: Ameshindwa kupata nafasi ya kudumu kikosini, hali inayoweza kupelekea kuondoka kwake.
- Clatous Chama: Licha ya kuhusika katika mabao 16 msimu huu, amepata muda mdogo uwanjani. Uwezekano wa kuondoka ni mkubwa.
- Yao Kouassi: Majeruhi wa muda mrefu, amecheza mechi saba tu. Nafasi yake tayari imechukuliwa na Israel Mwenda.
- Djigui Diarra: Mkataba wake unamalizika Juni 30, huku hatma yake ikiwa bado haijulikani.
Wachezaji Wanaotajwa Kuongeza Mkataba Yanga SC
Maxi Nzengeli – DR Congo
Nzengeli amekuwa mchezaji muhimu wa Yanga msimu huu akifunga mabao 5 na kutoa asisti 7. Tayari ameongeza mkataba hadi 2027.
Khalid Aucho – Uganda
Kiungo mkabaji na nahodha wa Uganda ameendelea kuwa nguzo ya Yanga katikati ya uwanja. Mazungumzo ya kuongeza mkataba bado yanaendelea.
Pacome Zouzoua – Ivory Coast
Zouzoua ameongoza kwa asisti msimu huu (8) na kufunga mabao 7. Tayari amefikia makubaliano ya kuongeza mkataba hadi 2027.
Dickson Job – Tanzania
Nahodha msaidizi na beki tegemezi ameongeza mkataba hadi 2027 licha ya Simba SC kuwa na nia ya kumsajili.
Mudathir Yahya – Tanzania
Amejihakikishia nafasi kikosini msimu huu. Ingawa mkataba wake unaelekea ukingoni, mazungumzo ya kumbakiza yanaendelea huku Azam FC wakitajwa kummezea mate.
Hitimisho: Yanga Yasuka Kikosi Kipya kwa Maono Mapya
Tetesi za usajili Yanga SC 2025/2026 zinaashiria mabadiliko makubwa na mkakati mpya wa ushindani. Kupoteza nyota kama Aziz Ki na sintofahamu juu ya baadhi ya wachezaji waliopo kunalazimu uongozi kufanya maamuzi ya haraka. Mashabiki wa Yanga wanaendelea kufuatilia kila hatua kwa matumaini ya kuona kikosi kipya kinachoweza kuleta mafanikio makubwa msimu ujao.
🔔 Unatafuta Nafasi za Kazi? Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya ajira kila siku!
🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!