Michezo

Viingilio Mechi ya Yanga vs Simba – 25 Juni 2025

VIINGILIO Yanga vs Simba 25 June 2025

Viingilio Mechi ya Yanga vs Simba Juni 25, 2025

Viingilio Mechi ya Yanga vs Simba Juni 25: Yanga SC imethibitisha viingilio rasmi vya mechi yake ya Ligi Kuu NBC dhidi ya Simba SC, itakayopigwa Jumatano ya tarehe 25 Juni 2025 saa 11:00 jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam. Hii ni moja ya mechi zinazovuta hisia kubwa zaidi nchini, maarufu kama Kariakoo Derby.

Eneo la Mchezo na Muda wa Kuanza

Pambano hili litachezwa katika dimba la Benjamin Mkapa, likianza saa 11 jioni. Mashabiki wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu zao kwenye mchezo huu wa kihistoria.

VIINGILIO Yanga vs Simba 25 June 2025

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Yanga SC, viingilio vya mchezo huo vitakuwa kama ifuatavyo:

Mzunguko

  • TSh 5,000

Orange

  • TSh 10,000

VIP C

  • TSh 20,000

VIP B

  • TSh 30,000

VIP A

  • TSh 50,000Tiketi zimekwisha

Tiketi za VIP A, ambazo ndizo za juu zaidi, tayari zimeuzwa zote, ishara ya jinsi mchezo huu unavyovutia mashabiki wengi na kuvunja rekodi kila mara.

VIINGILIO Yanga vs Simba 25 June 2025

Mashabiki Waaswa Kukata Tiketi Mapema

Yanga SC imewahimiza mashabiki wa timu zote kuhakikisha wananunua tiketi mapema ili kuepuka usumbufu na msongamano siku ya mchezo. Kutokana na ukubwa wa mechi na idadi kubwa ya watu wanaotarajiwa kuhudhuria, hatua za mapema zitasaidia mashabiki kupata nafasi bora uwanjani.

🔔 Je? unatafuta Nafasi za Kazi? Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya ajira kila siku!

🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!