Klabu ya Yanga SC imetangaza rasmi vituo maalum vya kupatikana tiketi za Yanga Day 2025, tamasha litakalofanyika Ijumaa tarehe 12 Septemba 2025 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Vituo vya Tiketi za Yanga Day 2025 Jijini Dar es Salaam
Mashabiki wanaweza kupata tiketi zao kwenye vituo mbalimbali vikiwemo:
- Yanga SC – Jangwani
- Ubungo (Alphan Hinga, Jackson Kimambo, New Tech General Traders)
- Mbagala (Gitano Samweli, Sabana Business – Maji Matitu)
- Temeke (Mtemba Service Co.)
- Ilala (Khalfan Mohamed)
- Sinza/Kivukoni (Antonio Service)
- Leaders – Shirima Shop
- Dar Live – Karoshy Pamba
- Mikocheni – View Blue Skyline
- Gwambina Lounge – Gwambina
Vituo Nchi Nzima
Mbali na Dar es Salaam, mashabiki pia wanaweza kupata tiketi kupitia wasambazaji walioteuliwa kote nchini, ikiwemo Mkaluka Traders (Machinga Complex) na maduka ya TTCL.
Kwa mashabiki wa Yanga, hii ni nafasi ya kuhakikisha wanapata tiketi mapema ili kuepuka usumbufu siku ya tamasha.