Michezo

Wachezaji 15 wa Tembo Warriors Kwenda Burundi

Wachezaji 15 wa Tembo Warriors Kwenda Burundi

Wachezaji 15 Tembo Warriors kuelekea Burundi

Dar es Salaam: Shirikisho la Mpira wa Miguu kwa Watu Wenye Ulemavu Tanzania (TAFF) limetangaza kikosi cha wachezaji 15 wa Tembo Warriors watakaoshiriki mashindano ya Baraza la Vyama vya Michezo Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) yatakayofanyika nchini Burundi kuanzia Septemba 8 hadi 14, 2025.

Kikosi cha Tembo Warriors

Mkurugenzi wa Ufundi wa TAFF, Shabani Msangi, ametangaza majina ya wachezaji walioteuliwa na kuthibitisha kuwa wote wamekidhi vigezo vya kushiriki michuano hiyo. Wachezaji waliochaguliwa ni:

  • Ally Juma
  • Bashra Alombile
  • Hassan Vuai
  • Abdulkareem Khalifa
  • Richard Swai
  • Emmanuel Mrefu
  • Modrick Mohamed
  • Ally Cheche
  • Juma Kidevu
  • Rojas Vicent
  • Kassim Mbarouk
  • Frank Ngairo
  • Julius Keika
  • Salim Chambon
  • Salehe Mwipi

Benchi la Ufundi

Msangi pia alithibitisha kuwa Kocha Ivo Mapunda ataongoza benchi la ufundi la kikosi hicho katika mashindano hayo.

“Tunatarajia mashindano yenye ushindani mkubwa na tunaamini kikosi hiki kilichochanganya uzoefu na vipaji kitaipeperusha vyema bendera ya taifa,” alisema Msangi.


Tembo Warriors sasa wanajiandaa kwa safari ya Burundi wakilenga kufanya historia kwenye michuano ya CECAFA 2025.

🔔 Kwa habari mpya za Michezo. Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya michezo kila siku!
🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!