WAFUNGAJI BORA NBC Premier League 2024/2025 Vinara wa Magoli
WAFUNGAJI BORA NBC Premier League 2024/2025. Katika msimu wa 2024/2025 wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, mashindano ya kuwania Kiatu cha Dhahabu yamekuwa ya kusisimua kwa mashabiki na wapenda soka. Wachezaji kutoka vilabu mbalimbali wameonyesha kiwango kikubwa cha ushindani wakisaka nafasi ya kuwa mfungaji bora wa msimu huu.
Msimu huu umejaa majina makubwa kama vile Jean Charles Ahoua wa Simba SC, anayekamata nafasi ya juu kwa sasa kwa mabao 16, pamoja na wakali kutoka Yanga SC, Azam FC, Singida Black Stars na timu nyingine zinazotoa ushindani mkali.
Wafungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara
Vinara wa Ufungaji:
Kwa mashabiki wa soka na wadau wa mchezo huu pendwa, hii hapa ni orodha kamili ya wafungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC hadi kufikia tarehe 18 Juni 2025:
#NO: | Mchezaji | Timu | Utaifa | Magoli |
---|---|---|---|---|
1. | Jean Ahoua | Simba | Ivory Coast | 16 |
2. | Jonathan Sowah | Singida BS | Ghana | 13 |
3. | Steven Mukwala | Simba | Uganda | 13 |
4. | Leonel Ateba | Simba | Cameroon | 13 |
5. | Clement Mzize | Young Africans | Tanzania | 13 |
6. | Prince Dube | Young Africans | Zimbabwe | 13 |
7. | Gibril Sillah | Azam | Gambia | 11 |
8. | Pacome Zouzoua | Young Africans | Ivory Coast | 11 |
9. | Elvis Rupia | Singida BS | Kenya | 10 |
10. | Ki Stephane Aziz | Young Africans | Burkina Faso | 9 |
11. | Peter Lwasa | Kagera Sugar | Uganda | 8 |
12. | Nassor Saadun | Azam | Tanzania | 8 |
13. | Paul Peter | Dodoma Jiji | Tanzania | 8 |
14. | Mathew Tegisi | Pamba Jiji | Kenya | 7 |
15. | Iddi Kipagwile | Dodoma Jiji | Tanzania | 7 |
16. | Offen Chikola | Tabora UTD | Tanzania | 7 |
17. | Lusajo Mwaikenda | Azam | Tanzania | 6 |
18. | Max Nzengeli | Young Africans | DR Congo | 6 |
19. | Marouf Tchakei | Singida BS | Togo | 6 |
20. | Edward Songo | JKT Tanzania | Tanzania | 6 |
21. | William Edgar | Fountain Gate | Tanzania | 6 |
22. | Clatous Chama | Young Africans | Zambia | 6 |
23. | Heritier Makambo | Tabora UTD | DR Congo | 6 |
24. | Selemani Mwalimu | Fountain Gate | Tanzania | 6 |
25. | Ibrahim Abdulla Bacca | Young Africans | Tanzania | 5 |
26. | Zidane Ally | Dodoma Jiji | Tanzania | 5 |
27. | Maabad Maulid | Coastal Union | Tanzania | 5 |
28. | Elie Mokono | Fountain Gate | Burundi | 5 |
29. | Erasto Nyoni | Namungo | Tanzania | 5 |
30. | Iddy Selemani | Azam | Tanzania | 5 |
Wanaofuatia kwia karibu (8 hadi 5 Mabao):
Wachezaji kama Peter Lwasa (Kagera Sugar), Offen Chikola (Tabora United), na Nassor Saadun (Azam FC) wamefunga mabao 8 kila mmoja. Wengine kama Seleman Mwalimu, Idd Nado, na Paul Peter wana mabao 6 huku kundi kubwa likiwa na mabao 5.
Wenye Mabao 4 na Chini:
Kundi hili lina majina mengi kutoka vilabu vyote vikubwa na vidogo. Miongoni mwao ni Feisal Salum (Azam FC), Fabrice Ngoma (Simba SC), Kennedy Musonda (Yanga SC), na wengine wengi wanaotegemewa kuongeza idadi ya mabao katika mechi zijazo.
Ushindani Mkali wa Kiatu cha Dhahabu
Kwa kila mzunguko wa ligi, orodha ya wafungaji hubadilika huku wachezaji wakiongeza juhudi kuhakikisha wanakuwa miongoni mwa vinara wa magoli. Kwa sasa, Ahoua anaonekana kuwa kwenye njia sahihi, lakini ushindani bado uko wazi.
Mashabiki wanatarajia kushuhudia mabao ya kuvutia kutoka kwa wachezaji wanaowania tuzo hii ya kifahari. Bila shaka, mechi zilizosalia zitakuwa na msisimko mkubwa.
🔔 Unatafuta Nafasi za Kazi? Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya ajira kila siku!
🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!