Kuitwa Kazini Tume ya Utumishi wa Mahakama 2025
Tume ya Utumishi wa Mahakama (JSC) imetangaza majina ya waombaji waliofanikiwa kufaulu usaili na kuchaguliwa kuajiriwa kwenye Utumishi wa Mahakama kwa mwaka 2025. Tangazo hili linahusu nafasi mbalimbali zilizotangazwa tarehe 03 Juni 2025.
Maelekezo kwa Waliofanikiwa
Waombaji waliopata nafasi wametakiwa kuangalia barua zao za ajira kupitia baruapepe (Email) na kufuata maelekezo yaliyomo ndani yake. Hii ni hatua muhimu ya kuthibitisha ajira zao na kuanza majukumu mapya ndani ya Utumishi wa Mahakama.
Kwa Wasiofanikiwa
Kwa wale ambao majina yao hayajaorodheshwa kwenye tangazo hili, wafahamu kuwa kwa sasa hawakubahatika kupata ajira kwa nafasi walizoomba.
Orodha ya Walioitwa Kazini
Tume imeweka orodha ya majina ya walioitwa kazini kwa kada mbalimbali. Waombaji wanaweza kupakua orodha hiyo kupitia kiunganishi rasmi: