Yakoub Suleiman Ni Usajili Mpya wa Simba SC
Klabu ya Simba SC imekamilisha usajili wa mlinda mlango wa Taifa Stars, Yakoub Suleiman, kutoka JKT Tanzania FC kwa mkataba wa miaka mitatu.
Mlinda Mlango Namba Moja Taifa Stars
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 23 ndiye mlinda mlango wa kwanza wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, na usajili wake ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Simba SC baada ya makubaliano na JKT Tanzania kufikiwa.
Rekodi ya Yakoub Suleiman
Katika msimu wa 2024/2025, Yakoub Suleiman alikuwa mhimili wa safu ya ulinzi ya JKT Tanzania, akimaliza na clean sheet 8 na kuisaidia timu hiyo kumaliza nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC.
Kuimarisha Safu ya Ulinzi Simba
Yakoub anajiunga na kikosi cha Simba SC akitarajiwa kushirikiana na Moussa Camara, ambaye msimu uliopita aliibuka kipa bora wa ligi baada ya kuweka rekodi ya clean sheet 19. Usajili huu unaimarisha zaidi safu ya ulinzi ya Wekundu wa Msimbazi kuelekea msimu mpya wa 2025/2026.
Kwa ujio wa Yakoub Suleiman, Simba SC inaongeza nguvu kubwa kwenye lango lake ikilenga mafanikio ndani na nje ya Tanzania.
🔔 Kwa habari mpya za Michezo. Jiunge na Watanzania wengine kupitia WHATSAPP CHANNEL kwa matangazo ya michezo kila siku!
🌐 Tembelea Habari Wise kwa habari mpya kila siku!